|
Charles
Guzo
This testimony in English
Bwana
asifiwe! Ninampa sifa na utukufu Bwana wetu Yesu Kristo, aishie
milele na milele ambaye ameniwezesha kupata haki ya kuishi milele
na milele. Yeye ni mwokozi wangu na amenisamehe dhambi zangu zote
za kutokea udogo hadi sasa, na amelifuta jina langu katika kitabu
cha hukumu na kuliandika kwenye kitabu cha uzima wa milele. Sasa
ameniweka huru, tena huru kwelikweli.
Nikiwa
katika Watangatanga Band baada ya kutoka Sparrows Band, nilikuwa
nikipiga miziki ya jazz kule The New Hotel Tanga Tanzania.
Nilikuwa nikishiriki kupiga drums pamoja na Paul
Box raia wa Marekani. Rafiki yangu Paul yuko Marekani siku
hizi na ni profesa katika Chuo Kikuu cha Utah. Nimewasiliana naye
kupitia mtandao huu wa amefufuka.com nilivyo sign guest book.
Alinipata akaniuliza kama ni mimi mwenyewe?
Wakati
mwingine nilikuwa nikipiga gitaa na kuimba nyimbo za Kiingereza
na Kiswahili, na mara nyingine nilicheza bass guiter. Band hii
ilikuwa kubwa na maarufu Tanzania kwa sababu ilikuwa na wanamuziki
wazungu wengi kuliko waswahili, na vyombo vilikuwa vya hali ya
juu sana kwa ubora na gharama.
Hata
nilipoenda Bugando Mwanza hapa hapa Tanzania kusomea Medical Laboratory
Technology, niliweza kupiga muziki part-time kwenye hotel ya kitalii
iitwayo New Mwanza Hotel. Nilikuwa naimba nyimbo za jazz huku
nikipiga galatoni (acostic guitar).
Niliimba
kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahili na lugha zinginezo kwa njia
ya kunakili kwa mfano; Kihispania, Kifaransa, Kiarabu, Kihindi,
na Kilatini. Baada ya kurudi masomoni, niliimarisha vyombo vyangu
vya muziki maana baadhi ya vyombo nilipewa kutoka Watangatanga
Band. Kiongozi wa band hii alikuwa anaitwa Erling
Petersern. Huyu ninamkumbuka kwani alikuwa mwalimu wangu wa
guiter chords na Paul Box alinifundisha ku-roll drums. Hata hivyo,
marehemu Henry Mdimu, kiongozi wa Sparrows Band na mpuliza sax
alinifundisha nyimbo za zamani lakini mbinu za uimbaji nilipata
kwa Watangatanga Band.
Jinsi
nilivyookoka!
Nilikodishwa vyombo vyangu vya muziki kwenye mkutano wa injili.
Fundi mitambo alikuwa mimi mwenyewe kwa hivyo injili ambayo nilikuwa
naikimbia kila mara ilibidi niisikie. Mhubiri alitoka Kenya na
jina lake ni Paulo Mbugwa. Huwa anahubiri vipindi vya redioni
huko Kenya. Mwenyeji wake alikuwa Mchungaji George Barnali E.A.G.T.
Makorora Tanga.
Siku
ya kwanza, injili iliingia moyoni mwangu na machozi ya furaha
na matumaini ya uzima wa milele yakajaa moyoni mwangu lakini nilijizuia.
Siku
ya pili, nilishindwa kujizuia. Ilikuwa Mwezi wa Tisa 1994. Mhubiri
Paulo Mbugwa alipouliza nani anahitaji kumpa Yesu maisha yake,
nilinyoosha mikono yangu yote miwili na kutoka mbele. Kwa kweli,
wahubiri walidhani labda sikuwa nimeelewa. Hivyo basi, walirudia
tena mara ya pili ili kuhakikisha. 
Ilipoonekana
nilikuwa nimeamua kuokoka, ilikuwa ni sifa kwa
Yesu mwana muziki kuokoka. Sasa nina mke na watoto watano.
Baada
ya kuokoka badiliko langu lilimvuta mke wangu Elizabeth Kitiku
naye akaokoka katika wiki moja. Yeye ni Afisa muuguzi katika Hospitali
ya Mkoa ya Bombo. Tulianza kujuana tulipokuwa masomoni Bugando
Medical Centre.
Tulikuwa
ndani ya nyumba hatuna fedha wakatokea wanamuziki wa duniani wakitaka
kukodi vyombo vya muziki kwa siku moja kwa kiasi cha shilingi
40,000/= nilikataa kwa vile ndani nilihukumiwa. Lakini baadaye
ile gari ambayo tungesafiri nayo ikapata ajali mbaya sana kuna
waliokufa na kuvunjika.
Jambo
lingine: nilitumiwa galatoni mpya bila kutarajia, mke wangu akashangaa.
Naomba Mwenyezi Mungu ambariki sana Dan
Wolf Meyrowitsch.
Jambo
lingine niliuziwa darubini nzuri (microscope) kwenye idara yangu
kwa bei ya writenoff (boarded items) kwa shilingi 1,000/= tu.
Huu ulikuwa muujiza mkubwa! Majirani wakawa wanahitaji huduma
ikabidi nikatafute na reagent za kupimia. Siku ya kwanza tu ile
1,000/= ikarudi mara kumi! Huu ulikuwa muujiza wa Bwana.
Ikawa
sinywi tena pombe akazidisha upendo wake juu yangu akagundua maisha
ya wokovu yana raha akaniambia niende naye kwa mchungaji Geoge
Barnali ndipo mambo yakawa mazuri zaidi. Watoto wetu walivalishwa
ma-hirizi yakachomwa moto tukawa huru hakuna kuogopa wachawi tena.
Naishi
hapa hapa Tanga na ninashiriki katika kanisa la Calvary Assemblies
of God. Wachungaji wangu ni Apostle
Dustan Maboya na Kundael Mmari.
--
Charles Guzo
To contact Charles, please write
to us for his contact.
There is too much email abuse by spammers to give it here.
Charles
Guzo ni mtumishi wa Mungu na mwimbaji wa nyimbo za kumsifu Mungu.
Baadhi ya nyimbo alizotunga ni (Charles Guzo is a servant of
God and a gospel singer. Some of the songs he has written are):
- Baba
Yetu
- Haleluya
- Utaokoka
|