WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Karibu katika ukumbi wa mijadala hapa amefufuka.com. Lugha ya msingi katika ukumbi huu ni Kiswahili. Huu ukiwa ni ukumbi wa Kikristo, tunatarajia tutazingatia lugha nadhifu na kuonyeshana heshima kwa wote licha ya kutofautiana kimaoni.

WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby martha.mapalala » Wed Apr 03, 2013 5:51 pm

nawasalimu nyote katika Jina la Yesu Kristo.

tumekuwa kimya sana. sijui tumechoka sana.! tusichoke. tuamke na tujadiliane. yapo mambo mengi yatupasayo kushirikishana kila leo ili kuwekana macho. shetani anazunguka sana kuwatia uzito watoto wa Mungu. sisi tunaosikia leo na tukatae kugandamizwa na adui. tuamke na kwa pamoja tushirikiane upya kumpindua shetani na hila zake zote.

pamoja ndani ya ushirika wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

binafsi nimewamiss sana na nawaombeni kwa upendo kabisa tukutane katika jukwaa letu la AMEFUFUKA MAJADILIANO/DISCUSSIONS.

BARIKIWA!
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby sinmm » Sat Apr 06, 2013 2:04 pm

Dada Martha asante na Mungu akubariki. Kweli kuna mambo mengi ya kujadili, mafunzo mengi ya kujifunza, na shuhuda nyingi tu za kutoa. Ila wapendwa tumechoka au shughuli zinatuzuia. Nimefikiri sana kuhusu jambo hili na kuona labda ni bora kufunga foramu hii. Yaliyomo yatabaki na watu wataweza kufikia kila topic na posts zote ila hakutakuwa na nafasi ya kupost tena. Yaani iwe kama archive tu.

Unaonaje?
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby martha.mapalala » Sun Apr 14, 2013 6:42 pm

hapana kaka Mark. Sikubaliani na suala hili. Kwani hakuna njia yoyote nyingine ambayo tutaitumia ili kuitangaza amefufuka majadiliano? Wale wapendwa wana amefufuka wote hatuwezi kuwafikia kwa njia ya simu au ujumbe mfupi wa maneno namba zao zinaweza patikana? Mimi sifurahishwi na jinsi tulivyolala. Kaka Mark toa mwongozo.
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby Guzo » Mon Apr 15, 2013 11:34 am

hapana usiifunge tafadhali, Mark endelea kunivumilia! kuanzia leo nitakuwepo kila siku nikijadili hata kama ni sisi watatu bora tusiweke gap.
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby sinmm » Tue Apr 16, 2013 1:30 pm

Asanteni kwa mawaitha, nitafanya mlivyopendekeza. Ukumbi utabaki wazi.
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby sinmm » Tue Apr 16, 2013 1:44 pm

martha.mapalala wrote:Wale wapendwa wana amefufuka wote hatuwezi kuwafikia kwa njia ya simu au ujumbe mfupi wa maneno namba zao zinaweza patikana? Mimi sifurahishwi na jinsi tulivyolala. Kaka Mark toa mwongozo.


Dada Martha, simu hatuna. Dada Lydia alihamia Pretoria nilikuwa na namba yake ya Msumbiji. Yake dada Ntac nilikuwa nayo ila kitambo sasa lakini tunawasiliana kwa email. Dada Upendo na ndugu wengine nimewatumia email wote. Labda tuanze kualika wapendwa wapya wajisajili.

Kuna topics nyingi ambazo ningependa tujadili na nitazileta hivi karibuni baada ya kumaliza shughuli fulani kazini. Inabidi tuwe macho kwa maana Ibilisi na jeshi lake wanachapa kazi usiku mchana. Mlisikia habari za wachawi walionaswa Mwanza. Nilisikia watu wengine wakisema kuwa wale wachawi walikuwa wasanii tu waliotumiwa na lile kanisa kwa kusudi la kujaza kanisa. Ukweli umefichika japo uko tu wazi kwa walio na macho yanayoona.
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby Guzo » Thu Apr 18, 2013 10:04 am

Hata huku Tanga wapinga kristo wapo, wasioamini habari za miujiza siwezi kusema mengi ila nikisema naona kama nawasaidia kufanikisha kazi yao.wame wasema watumishi wengi sana lakini hatima yao ipo!
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby sinmm » Sat Jul 27, 2013 10:04 pm

Dada Martha alitoa point, tuamke. Tumelala sana, kisha usingizi mzito ukamdaka yeye mwenyewe. Dada Martha, upo? Amka!
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: WAPENDWA WA AMEFUFUKA MAJADILIANO-TUAMKE. TUMELALA SANA.

Postby Guzo » Mon Jul 29, 2013 4:46 pm

sinmm wrote:Dada Martha alitoa point, tuamke. Tumelala sana, kisha usingizi mzito ukamdaka yeye mwenyewe. Dada Martha, upo? Amka!

kwa kweli mimi nipo.
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania


Return to ::Matangazo::

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 0 guests

cron