KIJANA NA CHANGAMOTO YA HALI HALISI YA MAISHA

Ukumbi wa vijana wakristo kujadili mambo yanayowahusu wao katika jamii; kwa mfano, elimu, uchumba, uinjilisti, ukimwi, na kadhalika. Karibuni, vijana.

Re: KIJANA NA CHANGAMOTO YA HALI HALISI YA MAISHA

Postby Guzo » Thu Mar 29, 2012 7:03 pm

Mimi nathani hakumwangalia kama petro kwa wakati ule alimwangalia shetani alikuwa ndani yake ili avuruge mpango wa Mungu , vinginevyo kusingekuwepo wokovu au wasemaje?
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Re: KIJANA NA CHANGAMOTO YA HALI HALISI YA MAISHA

Postby sinmm » Thu Mar 29, 2012 7:16 pm

Guzo wrote:Mimi nathani hakumwangalia kama petro kwa wakati ule alimwangalia shetani alikuwa ndani yake ili avuruge mpango wa Mungu , vinginevyo kusingekuwepo wokovu au wasemaje?

Kweli kabisa, alimwangalia shetani aliyekuwa amejificha kando au ndani ya Petro. Funzo hapa ni kuwa tuwe waangalifu maana shetani akipata pengo, anaweza akamwingia mtu yeyote. Tusimpe nafasi ya kupenya maishani mwetu.
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: KIJANA NA CHANGAMOTO YA HALI HALISI YA MAISHA

Postby Guzo » Thu Mar 29, 2012 7:23 pm

sinmm wrote:
Guzo wrote:Mimi nathani hakumwangalia kama petro kwa wakati ule alimwangalia shetani alikuwa ndani yake ili avuruge mpango wa Mungu , vinginevyo kusingekuwepo wokovu au wasemaje?

Kweli kabisa, alimwangalia shetani aliyekuwa amejificha kando au ndani ya Petro. Funzo hapa ni kuwa tuwe waangalifu maana shetani akipata pengo, anaweza akamwingia mtu yeyote. Tusimpe nafasi ya kupenya maishani mwetu.

si unajua kuteswa kwake Yesu ni furaha?, kumwaga damu yake msalabani, na kufa kwake? lakini ukiingia ki dini unasikitika na kusema Yesu alikuwa na uwezo hata kuwaangamiza wale wote waliomtesa !
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Re: KIJANA NA CHANGAMOTO YA HALI HALISI YA MAISHA

Postby Lydia » Fri Mar 30, 2012 9:48 am

Hapa Kaka zangu mna hoja nzuri sana, naona mengi kuhusu Petro ambayo twaweza kujifunza katika maisha yetu ya leo. kama Petro alikuwa anakosea lakini hakuacha kuwa mwanafunzi wa Yesu, aliomba kutembea juu ya maji akapewa kibali, akiwa anamuona Yesu uso kwa uso bado imani yake ilitindika akaanza kuzama. Na bado siku ilifika BWANA Yesu alimwambia juu yako wewe Petro nitajenga kanisa

sisi leo tunawaangalia sana watumishi akifanya kosa fulani tu tunaona ameshaacha kabisa kuwa mtumishi hata akihubiri hatutaki kumsikiliza kumbe yeye alishatengeneza na Mungu zamani.
HALELUYA
User avatar
Lydia
Regular Member
 
Posts: 328
Joined: Fri Apr 29, 2005 7:11 am
Location: Mozambique

Re: KIJANA NA CHANGAMOTO YA HALI HALISI YA MAISHA

Postby Guzo » Fri Mar 30, 2012 6:01 pm

Hata mfalme Daudi!,unajua hawa watu wanaopenda kutubu, kujitakasa, kujutia dhambi,kujishusha si watu wa kawaida.!mfalme Daudi juu ya kuharibu kote Mungu alimwiita moyo wake ni myo wa Mungu na hatimaye Yesu alitoka katika ukoo wake kupitia ahadi zake tokea Ibrahim. Kweli Lydia usiombe ukakutwa na mwanadamu!he! utakiona cha mtema kuni!
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Previous

Return to Baraza la Vijana

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest

cron