MKRISTO NA DUNIA

Jadili mambo yanayotuhusu sisi wakristo, kwa mfano, jinsi ya kuishi baada ya kumpokea Bwana Yesu kama mwokozi, na kadhalika.

MKRISTO NA DUNIA

Postby martha.mapalala » Fri Nov 18, 2011 8:02 am

Praise the Lord Jesus.

Nina swali naomba mnisaidie. swali lenyewe ni hili.

....Je, mkristo hasa yule aliyeokoka anaruhusiwa kutazama filamu, tamthiliya kama hizi zinazoonyeshwa katika runinga? mfano; the second chance, la revenche e.t. c.

Nimeuliza coz mimi nazipenda sana. sasa sometimes najikuta nakuwa mtumwa wa hivi vitu. i just value them that i can't sleep without getting a single dose of tamthiliya. matokeo yake hata muda ambao nampa Mungu kwa siku haufanani na huu ambao nampatia tamthilia. Tfadhali naomba mnisaidie kama ni nzuri kuzitazama au la kwa kristo aliyeokoka.

BARIKIWA!
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby sinmm » Mon Nov 21, 2011 12:48 pm

Filamu na tamthilia zinazoonyeshwa kwenye runinga zinamadhumuni ya kuburudisha na mara nyingine kuelimisha. Nilipokuwa chuo kikuu nilikuwa na rafiki mmoja aliyeniambia kuwa yeye hakujua kupiga domo. Mazungumzo yake yalizungukia shuhuda, Neno la Mungu, na maongezi ya kutia moyo. Alijaribu alivyoweza kujikinga na mazingira na maongezi ambayo yangemfanya atende dhambi.

Siko Tanzania na sijui the second chance, la revenche na vipindi vingine vina mada gani. Hata hivyo, tamthilia nyingi zinazokwenda kwa muda mrefu (miezi na hata miaka) zina lengo la kumteka mtu na kumfanya mfungwa. Zaidi ya miaka 10 iliyopita tulikuwa watumwa wa kipindi cha "The Blond & The Beautiful". Nilipokosa kuona hata sehemu moja tu ya kipindi hiki nilijisikia vibaya sana; niliumwa. Halafu waandishi wa riwaya hizi walikuwa na tabia ya kumtia mtu hamu mwishoni mwa kipindi ili mtu afanye vyovyote ili asikose kuona kipindi kilichofuatilia. "What will happen next?"

Wahusika kwenye vipindi hivi walitenda madhambi ambayo mtazamaji (hata wale walokole waliotekwa nyara) walitupilia mbali wakisingizia kuwa ilikuwa ni tamthilia tu. Dada wengi sana walikabwa na wamekabwa kwenye mtego huu. Namshukuru Mungu aliyavunja minyororo iliyotufunga kwenye sehemu hii. Filamu na tamthiliya hizi kwenye runinga ni kama mvinyo (divai) na hata madawa ya kulevya. Ukishaanza ni vigumu kuacha. Badala yake, mtume Paulo anatushauri tukomboe wakati kwa sababu siku hizi ni MBAYA sana:

Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima. Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana. Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu. Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu. Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo. (Waefeso 5:16-21)
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby martha.mapalala » Mon Nov 21, 2011 4:23 pm

sinmm wrote:Filamu na tamthilia zinazoonyeshwa kwenye runinga zinamadhumuni ya kuburudisha na mara nyingine kuelimisha. Nilipokuwa chuo kikuu nilikuwa na rafiki mmoja aliyeniambia kuwa yeye hakujua kupiga domo. Mazungumzo yake yalizungukia shuhuda, Neno la Mungu, na maongezi ya kutia moyo. Alijaribu alivyoweza kujikinga na mazingira na maongezi ambayo yangemfanya atende dhambi.

Siko Tanzania na sijui the second chance, la revenche na vipindi vingine vina mada gani. Hata hivyo, tamthilia nyingi zinazokwenya kwa muda mrefu (miezi na hata miaka) zina lengo la kumteka mtu na kumfanya mfungwa. Zaidi ya miaka 10 iliyopita tulikuwa watumwa wa kipindi cha "The Blond & The Beautiful". Nilipokosa kuona hata sehemu moja tu ya kipindi hiki nilijisikia vibaya sana; niliumwa. Halafu waandishi wa riwaya hizi walikuwa na tabia ya kumtia mtu hamu mwishoni mwa kipindi ili mtu afanye vyovyote ili asikose kuona kipindi kilichofuatilia. "What will happen next?"

Wahusika kwenye vipindi hivi walitenda madhambi ambayo mtazamaji (hata wale walokole waliotekwa nyara) walitupilia mbali wakisingizia kuwa ilikuwa ni tamthilia tu. Dada wengi sana walikabwa na wamekabwa kwenye mtego huu. Namshukuru Mungu aliyavunja minyororo iliyotufunga kwenye sehemu hii. Filamu na tamthiliya hizi kwenye runinga ni kama mvinyo (divai) na hata madawa ya kulevya. Ukishaanza ni vigumu kuacha. Badala yake, mtume Paulo anatushauri tukomboe wakati kwa sababu siku hizi ni MBAYA sana:

Basi, muwe waangalifu jinsi mnavyoishi: Msiishi kama wapumbavu, bali kama wenye hekima. Tumieni vizuri muda mlio nao maana siku hizi ni mbaya. Kwa hiyo, msiwe wapumbavu, bali jaribuni kujua matakwa ya Bwana. Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu. Zungumzeni kwa maneno ya Zaburi, nyimbo na tenzi za kiroho; mwimbieni Bwana nyimbo na zaburi kwa shukrani mioyoni mwenu. Mshukuruni Mungu Baba daima kwa ajili ya yote, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya kumcha Kristo. (Waefeso 5:16-21)

Thanks Sinmm. Umenifungua ktk huu mnyororo kwani maneno ya mtume Paulo kweli yamenitoa usingizini.
Barikiwa Kaka!
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby Guzo » Wed Nov 30, 2011 2:29 pm

Kweli ni utumwa fulani mimi kuna tamthilia moja ilikuwa inaonyeshwa saa nne ya usiku (forbiden passion), basi nitazurura huko lakini ikifika saa nne sharp nipo nyumbani hata wakati mwingine nilikuwa internate cafe kwenye majadiliano humu www.amefufuka.com nakatisha unaona utumwa huo? ila Mungu yu mwema kuna kitu kilisababisha umeme ulikatika saa nne siku ya kwanza,siku ya pili nikasafiri! nikakosa mawasiliano ya kufuatilia ile tamthilia hadi leo!Kwa kweli hadi Mungu aingilie kati kunaushabiki fulani , ila namshukuru Mungu kwa habari ya mpira simo kabisa? maana kuna wengi wamezolewa na ushabiki wa mpira pia unaonaje kwa habari ya mpiranayo?
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby martha.mapalala » Thu Dec 01, 2011 9:41 am

Guzo wrote:Kweli ni utumwa fulani mimi kuna tamthilia moja ilikuwa inaonyeshwa saa nne ya usiku (forbiden passion), basi nitazurura huko lakini ikifika saa nne sharp nipo nyumbani hata wakati mwingine nilikuwa internate cafe kwenye majadiliano humu http://www.amefufuka.com nakatisha unaona utumwa huo? ila Mungu yu mwema kuna kitu kilisababisha umeme ulikatika saa nne siku ya kwanza,siku ya pili nikasafiri! nikakosa mawasiliano ya kufuatilia ile tamthilia hadi leo!Kwa kweli hadi Mungu aingilie kati kunaushabiki fulani , ila namshukuru Mungu kwa habari ya mpira simo kabisa? maana kuna wengi wamezolewa na ushabiki wa mpira pia unaonaje kwa habari ya mpiranayo?

Kaka Guzo ni kweli. kwa habari ya upepo wa mpira ndo usiseme. hata kama mpira utaonyeshwa majira ya usiku wa manane watu hawatalala hadi wametazama mechi hiyo. Hata usingizi kipindi hicho sijui huwa unakwenda wapi! macho huwa ni wazi mithili ya tochi inayowaka. Ni ngumu kumshawishi mtu kwenda ibadani isipokuwa kwa neema ya Mungu.
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby Guzo » Thu Dec 01, 2011 12:29 pm

martha.mapalala wrote:

Hata usingizi kipindi hicho sijui huwa unakwenda wapi! macho huwa ni wazi mithili ya tochi inayowaka.
Nimecheka, nimecheka! Macho huwa wazi mithili ya tochi!!, hata mimi nashangaa mpira mmoja tu wanaugombea! kuna jirani yetu maskini alifariki dunia kwa ajili ya mpira timu yake ilifungwa!.
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby martha.mapalala » Fri Dec 02, 2011 8:51 am

Guzo wrote:

sasa mimi nilipokuwa foam five na six nilikuwa nacheza football. na ilikuwa ni lazima. nilikuwa nacheza nafasi ya kipa. sasa shuleni kwetu ilikuwa ni lazima ucheze kama huchezi unapewa adhabu ya shimo urefu ni kimo chako na upana ni mikono yako mara mbili. kuliko adhaabu bora ucheze. nikawa mtumwa wa mpira wa miguu. ukirudi umechoka kuomba huwezi.
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby Lydia » Sat Dec 03, 2011 3:53 pm

Mmenichekesha sana na habari za mpira, mimi nilikuwa mtuma wa filam za kinigeria, nilikuwa nimezijaza nyumbani kwangu, kila siku nitaangalia mpaka usiku kama ni week endi kuanzia asubuhi. Mungu ni mwema kweli. Siku moja nilisikia sauti ikiniambia acha kuangalia hizi, nilikuwa sebuleni na wanangu, nikafikiri ni mawazo yangu, ilirudia mara ya pili nika ignore, mara ya tatu ilikuja sauti kabisa nikadhani hata watoto wamesikia kumbe hawakusikia, nilijiinua taratibu mpaka chumbani. Mungu alisema nataka kusema na wewe lazima uache kuangalia hizi, na Mungu alisema namimi.
HALELUYA
User avatar
Lydia
Regular Member
 
Posts: 328
Joined: Fri Apr 29, 2005 7:11 am
Location: Mozambique

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby martha.mapalala » Sun Dec 04, 2011 1:57 pm

Lydia wrote:Mmenichekesha sana na habari za mpira, mimi nilikuwa mtuma wa filam za kinigeria, nilikuwa nimezijaza nyumbani kwangu, kila siku nitaangalia mpaka usiku kama ni week endi kuanzia asubuhi. Mungu ni mwema kweli. Siku moja nilisikia sauti ikiniambia acha kuangalia hizi, nilikuwa sebuleni na wanangu, nikafikiri ni mawazo yangu, ilirudia mara ya pili nika ignore, mara ya tatu ilikuja sauti kabisa nikadhani hata watoto wamesikia kumbe hawakusikia, nilijiinua taratibu mpaka chumbani. Mungu alisema nataka kusema na wewe lazima uache kuangalia hizi, na Mungu alisema namimi.

amen! huu ni ushuhuda mzuri sana dada Lyidia. Mungu na azidi kusema nawe daima!

BARIKIWA!
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby sinmm » Mon Dec 05, 2011 11:04 am

Lydia wrote:Mmenichekesha sana na habari za mpira, mimi nilikuwa mtuma wa filam za kinigeria, nilikuwa nimezijaza nyumbani kwangu, kila siku nitaangalia mpaka usiku kama ni week endi kuanzia asubuhi. Mungu ni mwema kweli. Siku moja nilisikia sauti ikiniambia acha kuangalia hizi, nilikuwa sebuleni na wanangu, nikafikiri ni mawazo yangu, ilirudia mara ya pili nika ignore, mara ya tatu ilikuja sauti kabisa nikadhani hata watoto wamesikia kumbe hawakusikia, nilijiinua taratibu mpaka chumbani. Mungu alisema nataka kusema na wewe lazima uache kuangalia hizi, na Mungu alisema namimi.

Nakumbuka nilipewa filamu moja ya kinigeria inayoitwa The Price. Ilihadithia masaibu yaliyompata mchungaji mmoja. Niliipenda sana nikaiweka kwenye DVD (ilikuwakwenya kanda ya video) na hata hapa kwenye amefufuka.com. Niliiondoa punde dada Lydia aliponiambia kuhusu mtegu huu. Baadaye niligundua kuwa washiriki wengi kwenye filamu hiyo wali-act kwenya filamu nyingine za kidunia zilizokuwa na ulevi, uzinzi, nk.
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby martha.mapalala » Mon Dec 05, 2011 12:20 pm

sinmm wrote:

Mimi pia nilishaitazama THE PRICE ya kinigeria. Ni nzuri kwa mafundisho. Naomba MNISAIDIE; Je, kutazama filamu kwa ajili ya mafundisho either ya kijamii au ya kiimani bila kuhusisha nani kaigiza ni vibaya?
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby sinmm » Fri Dec 09, 2011 2:00 pm

martha.mapalala wrote:Mimi pia nilishaitazama THE PRICE ya kinigeria. Ni nzuri kwa mafundisho. Naomba MNISAIDIE; Je, kutazama filamu kwa ajili ya mafundisho either ya kijamii au ya kiimani bila kuhusisha nani kaigiza ni vibaya?

Dada Martha, inategemea. Na mkristo anapaswa kuwa mwangalifu sana siku hizi za mwisho. Itakuwa vizuri kujiuliza ni mafunzo yepi ya kijamii utakayopata kwenye filamu (husika) ambayo hutapata kwenye Biblia, kanisani, mikutano ya injili, kwenye mawasiliano na ndugu katika Kristo, nk. Nakumbuka nilipokuwa form two (zamani sana) tulioneshwa filamu moja ya karate kutoka Japan iliyoitwa "Snakes & Monkeys". Filamu ilipomalizika, wanafunzi wengi walikimbia uwanjani kuigiza waliyoona. Walitaambaa-taambaa nyasini kama nyoka na kutuka ruka kama nyani.

Ni vizuri au ni vibaya? Hapa nadhani mtu binafsi apaswa kuchukuwa uamuzi. Kwa mfano, wakristo wengi hatunywi pombe kwa sababu iliyo wazi lakini mtume Paulo alimwasa kijana Timotheo na kumwambia, "Usinywe maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara kwa mara." (1 Timotheo 5:23). Hivyo basi, tuwe macho tunapofanya uchaguzi kuhusu mambo haya kwa sababu siku ya mwisho tutatoa hesabu.

Binafsi naona kuwa ni vizuri kuchagua njia nyembamba na kujikinga na hizi filamu isipokuwa inapomlazimu mtu. Watu kadhaa wametoa maoni yao kwenye link ifuatayo kuhusu swali hili ila nilivyosema hapo juu, uamuzi wa mwisho ni wa mtu binafsi.

http://www.jashow.org/surveys/christian ... ar-movies/
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby Guzo » Fri Dec 09, 2011 8:27 pm

Postby Guzo » Fri Dec 09, 2011 8:45 pm

Naona lazima kuna adui anayo mikakati yake jiulize kwa nini muda hautoshi mambo ni mengi? kama ni hizo filamu usiseme zimejaa , magazeti , radio , tv, mialiko sasa! kikao cha harusi! mara kuna tamthilia ! achilia mazoezi ya viungo ha ta muda wa maombi hamna.
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Re: MKRISTO NA DUNIA

Postby martha.mapalala » Wed Dec 14, 2011 8:12 am

sinmm wrote:
martha.mapalala wrote:Mimi pia nilishaitazama THE PRICE ya kinigeria. Ni nzuri kwa mafundisho. Naomba MNISAIDIE; Je, kutazama filamu kwa ajili ya mafundisho either ya kijamii au ya kiimani bila kuhusisha nani kaigiza ni vibaya?

Dada Martha, inategemea. Na mkristo anapaswa kuwa mwangalifu sana siku hizi za mwisho. Itakuwa vizuri kujiuliza ni mafunzo yepi ya kijamii utakayopata kwenye filamu (husika) ambayo hutapata kwenye Biblia, kanisani, mikutano ya injili, kwenye mawasiliano na ndugu katika Kristo, nk. Nakumbuka nilipokuwa form two (zamani sana) tulioneshwa filamu moja ya karate kutoka Japan iliyoitwa "Snakes & Monkeys". Filamu ilipomalizika, wanafunzi wengi walikimbia uwanjani kuigiza waliyoona. Walitaambaa-taambaa nyasini kama nyoka na kutuka ruka kama nyani.

Ni vizuri au ni vibaya? Hapa nadhani mtu binafsi apaswa kuchukuwa uamuzi. Kwa mfano, wakristo wengi hatunywi pombe kwa sababu iliyo wazi lakini mtume Paulo alimwasa kijana Timotheo na kumwambia, "Usinywe maji tu, bali unywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lako, kwani unaugua mara kwa mara." (1 Timotheo 5:23). Hivyo basi, tuwe macho tunapofanya uchaguzi kuhusu mambo haya kwa sababu siku ya mwisho tutatoa hesabu.

http://www.jashow.org/surveys/christian ... ar-movies/

Ni kweli kabisa kaka Sinmm. ulivyosema ni kweli tupu. ni kweli tunapaswa kuwa waangalifu sana kwa siku hizi za mwisho.
Kaka Guzo ulivyosema ni kweli tupu. MAMBO NI MENGI LAKINI MUDA HAUTOSHI. "Hapa ndipo penye hekima. mwenye masikio na asikie"

Binafsi naona kuwa ni vizuri kuchagua njia nyembamba na kujikinga na hizi filamu isipokuwa inapomlazimu mtu. Watu kadhaa wametoa maoni yao kwenye link ifuatayo kuhusu swali hili ila nilivyosema hapo juu, uamuzi wa mwisho ni wa mtu binafsi.
Mimi ni mgeni katika nchi, Usinifiche maagizo yako. Zaburi 119:19
User avatar
martha.mapalala
Member
 
Posts: 94
Joined: Tue Sep 20, 2011 9:13 am
Location: Arusha, Tanzania

Next

Return to Maisha ya Kikristo

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 2 guests

cron