FUNGU LA KUMI

Jadili mambo yanayotuhusu sisi wakristo, kwa mfano, jinsi ya kuishi baada ya kumpokea Bwana Yesu kama mwokozi, na kadhalika.

FUNGU LA KUMI

Postby rebecca » Fri May 05, 2006 1:46 pm

Bwana yesu asifiwe wapendwa,
mimi nina swali moja lanitatiza,hivi tunapotoa fungu la kumi,ni lazima kwa wale waliotoa kusomwa na kusimama kanisani ili waombewe?
Si tunaambiwa tunapotoa hata mkono wako wa kushoto usijue,sasa iweje nitangazwe si siri yangu mimi na Mungu wangu?
Nisaidieni kwa hilo
Mbarikiwe,Bwana awape hekima zaidi!
rebecca
New member
 
Posts: 4
Joined: Tue Apr 25, 2006 8:05 am

Postby Lydia » Sat May 06, 2006 11:19 am

Rebecca, fungu la kumi ni agizo la Mungu au kwa maneno mengine ile ni kama kodi kila pato unalopata 10% sio yako ni ya Mungu. soma Malaki 3. unapotoa unatimiza agizo la Mungu sasa kusimamishwa kanisani na kuombewa inaweza kuwa ni utaratibu wa hilo kanisa lakini cha muhimu ni wewe kutoa na kabla hujatoa wewe peke yako mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kufanya kazi/biashara au chochote kilichokupa pato hilo, na umuombe Mungu aipokee sehemu yake maana usipotoa unamwibia Mungu.
HALELUYA
User avatar
Lydia
Regular Member
 
Posts: 328
Joined: Fri Apr 29, 2005 7:11 am
Location: Mozambique

Postby Samuel of Jesus » Tue May 09, 2006 10:40 am

Fungu la Kumi sio siri ni kitu cha wazi na ni lazima. Ni haki kuombewa na ukapata baraka zako. Hata kama sio kusimama kuombewa. Wengine wanaandika majina na Mtumishi anachukua hatua kukuombea kwa jina lako. Lazima fungu la kumi lijulikane sio vyema kutoa kwa siri.
Unajua kutoa fungu la kumi kunatakiwa moyo maana linaupinzani maana unaweza kushangaa unapokea mshahara na unapata tatizo hapo hapo na kutumia pesa zote. Lazima Kukuombea. husikwazike kubari kuombewa.
''The Yesterday, Today, Forever Christ''
*Baba Hulda*
User avatar
Samuel of Jesus
Regular Member
 
Posts: 354
Joined: Fri Sep 24, 2004 12:14 pm
Location: Arusha -Tanzania

Postby Guzo » Fri May 12, 2006 8:49 am

Wote mmesema vyema! ila mimi ninapozipata muda ule ule na mahali popote namtafuta mchungaji nampa ili nisije nikazila! wakati mwingine natoa kanisani pia kanisani kwetu wanautaratibu wa kuwaombea wanaotoa mafungu ya kumi wakati mwingine sitoki kutoa maana nilisha toa! watu wengine wanadhani sitoi! lakini Mungu ndiye anayejua.
Waefeso 2:8
User avatar
Guzo
Frequent Member
 
Posts: 1206
Joined: Tue Sep 07, 2004 8:15 pm
Location: Tanga, Tanzania

Postby sinmm » Fri May 12, 2006 12:45 pm

Kwa wanaokimudu Kiingereza, hebu someni yaliyoandikwa HAPA kuhusu mada hii.
User avatar
sinmm
Site Admin
 
Posts: 595
Joined: Mon Aug 16, 2004 9:01 pm
Location: Oslo

Postby Lydia » Fri May 12, 2006 2:35 pm

asante kaka Sinmm nimesoma na ninaona hapa;

In short we are not obliged to tithe. We are not blessed if we tithe and we are not cursed if we don't.kwa upande wangu sikubaliani na sentensi hii. 10% ni amri na tusipotoa tunamuibia Mungu, maana yake tumeiasi sheria mojawapo ya Mungu.
HALELUYA
User avatar
Lydia
Regular Member
 
Posts: 328
Joined: Fri Apr 29, 2005 7:11 am
Location: Mozambique

Postby paulm » Fri May 12, 2006 7:30 pm

swala la "Fungu la Kumi"

Tunaweza kulikabili swala la "Fungu la Kumi" kwa njia nyingi ili tuielewe vizuri.

Njia moja ni kuangalia Kazi aliyoimaliza Yesu Kalvari.

Je, kwa Neema, Yesu alichukua dhambi zetu? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua umaskini wetu ? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua udhaifu wetu ? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua magonjwa yetu ? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua kushindwa kwetu? Ndio

Ikiwa ni kwa Neema(grace), hakuna kazi tunayoweza kufanya ili tupate hivyo vitu ila kumwamini Yesu tu. Inawezekanaje katika ukombozi wetu kuwa baraka zingine zinakuja kwa neema na zingine zinakuja kwa matendo (works) ? Yesu alifanya kazi kamili na Neema na matendo(works) haziendi sambamba katika ukombozi wetu.

Kama tuko na ile mindset ya kwamba hatuwezi tukabarikiwa tusipotoa fungu la kumi, hio ni kazi (works). Neema na Kazi haziendi pamoja katika ukombozi wetu. Watu wengi wana hiyo "mindset" (fikira) kwamba "nitafanya nitakavyo, nitaishi maisha yangu nipendavyo" lakini nitatoa tu fungu la kumi na Mungu ataendelea kunibariki ama ni lazima nitoe "fungu la kumi" ili Bwani anibariki.

Ikiwa tuna hiyo "mindset", basi tumekosea lakini kama tunatoa fungu la kumi kubariki kazi ya Bwana basi hiyo ni sawa kabisa.

Baba yetu anataka kuondoa hii mindset. Maisha yetu yote ni yake. Kila kitu tulichonacho ni chake. Hakuna Baba anayemwabia mtoto wake ni lazima alipe ili amsaidie na ninaamini wachungaji wanaowambia watu kwamba watapata laana wisiotoa "fungu la kumi" wanamhuzunisha Bwana sana. Baba gani anataka watoto wake wamwone hivyo?

Njia ya kuelewa mada yoyote kwenye Biblia ni kuisoma mpaka unaelewa context yake. ktk Malachi, ni vizuri kusoma Malachi yote na kueielewa kabisa. Kulikuwa na ukame mkubwa ktk nchi hii na Bwana kwa kupitia Malachi aliwambia makosa yao.

Kwanza hawa watu walikuwa wakitoa "fungu la kumi" lakini walikuwa wanafanya mambo mengine mabaya yaliyomhuzunisha Bwana. Hata ile "fungu la kumi" wiliyotoa ilikuwa mbaya (Mal 1:14). Bwana alitaka watoe "fungu la Kumi" iwasaidie mayatima na wajane Mal 3:5. Je "fungu la kumi" linawasaidia mayatima, wageni na wajane siku hizi katika makanisa yetu? Mimi ninamini nikitoa "fungu langu la kumi" niwapelekee hawa wajane na mayatima bila kupitia kanisa, Baba anafurahi kuliko nipeleke hii fedha kwa makanisa wale hawaangalii maslahi ya wajane na mayatima.

Kwendelea na Malachi 3:10, ile baraka Bwana alisema atawapatia wakigeuza mienendo yao na kuleta "fungu la kumi" safi ilikuwa Mvua. kumbuka kulikuwa na ukame. Walikuwa wamemwibia Bwana wa njia ngani? Kwa kukosa kuleta "fungu la kumi" safi ili mayatima, wageni na wajane wasaidike.

Kumbuka pia maandao ya Bwana (Gods provision) ni kwa neema na neema pekee 2Cor 8:19.
kwa ufupi, ile "mindset" uliyonayo nayo unapotoa "fungu la kumi" ndio inayotambulisha kama ni vizuri au hapana.

Ahsante!!
User avatar
paulm
New member
 
Posts: 13
Joined: Fri Sep 24, 2004 11:25 am
Location: Nairobi, Kenya

Postby Upendo » Sat May 13, 2006 8:01 pm

Je "fungu la kumi" linawasaidia mayatima, wageni na wajane siku hizi katika makanisa yetu? Mimi ninamini nikitoa "fungu langu la kumi" niwapelekee hawa wajane na mayatima bila kupitia kanisa, Baba anafurahi kuliko nipeleke hii fedha kwa makanisa wale hawaangalii maslahi ya wajane na mayatima.


Hiyo ni kauli nzito, kwani wengi husema fungu la kumi ni kwa ajili ya wachungaji kwani wanatumikia madhabahuni na wanastahili kula kutoka hapo kama neno lilivyoagiza. Mnasemaje?[/b]
Shalom
User avatar
Upendo
Frequent Member
 
Posts: 605
Joined: Mon Sep 13, 2004 10:52 pm
Location: USA

Postby Berea » Sat May 13, 2006 11:41 pm

Upendo wrote: ... kama neno lilivyoagiza. Mnasemaje?


Fafanua tafadhali. Neno limeagiza wapi mambo hayo kuhusu FlK?
User avatar
Berea
New member
 
Posts: 28
Joined: Tue Mar 22, 2005 2:06 pm

Postby Samuel of Jesus » Tue May 16, 2006 11:22 am

Fungu la kumi ni la baba yako wa kiroho. Yule anayewajibika na maisha yako ya Kiroho. Maana hawana kazi zaidi ya kukuchunga wewe. Sio la yatima au wajane. Kwa yatima na wajane toa sadaka sio fungu la kumi.
''The Yesterday, Today, Forever Christ''
*Baba Hulda*
User avatar
Samuel of Jesus
Regular Member
 
Posts: 354
Joined: Fri Sep 24, 2004 12:14 pm
Location: Arusha -Tanzania

Postby Berea » Tue May 16, 2006 4:00 pm

Samuel of Jesus wrote:Fungu la kumi ni la baba yako wa kiroho. Yule anayewajibika na maisha yako ya Kiroho. Maana hawana kazi zaidi ya kukuchunga wewe. Sio la yatima au wajane. Kwa yatima na wajane toa sadaka sio fungu la kumi.

Lydia wrote:kwa upande wangu sikubaliani na sentensi hii. 10% ni amri na tusipotoa tunamuibia Mungu, maana yake tumeiasi sheria mojawapo ya Mungu.

Guzo wrote:Wote mmesema vyema! ila mimi ninapozipata muda ule ule na mahali popote namtafuta mchungaji nampa ili nisije nikazila!.


Kaka Samuel of Jesus, dada Lydia, na kaka Guzo, mimi nitawaelewa zaidi mkinipa andiko kutoka kwenye Biblia linayounga mkono mnayosema hapo juu. Je, mnafahamu kuwa wakatoliki wengi hawali nyama siku ya Ijumaa? Wengi alifundishwa kuwa Bwana Yesu alisulubiwa siku ya Ijumaa na hivyo ni 'hatia' kula nyama siku hiyo. Nitatoa mfano mwingine: "Remember the Sabbath day, to keep it holy. Six days you shall labor, and do all your work; but the seventh day is a Sabbath to The Lord your God; in it you shall not do any work, you, or your son, or your daughter, your manservant, or your maidservant, or your cattle, or the sojourner who is within your gates; for in six days The Lord made heaven and earth, the sea, and all that is in them, and rested the seventh day; therefore The Lord blessed the Sabbath day and hallowed it."

Hiyo ni amri ya nne ya Mungu kwa Musa na wanaIsraeli. Swali basi ni hili, wewe hufuata amri hii? Kama jibu ni hapana, sababu zako ni zipi? Tena, je nyumbani kwako nyinyi hupika chakula siku hii? Kama jibu ni ndio, kwa nini? Hiyo si nikuvunja amri ya nne? Umewahi kutembe siku hii ya Sabato? Kama jibu ni ndio, kwa mwendo wa umbali gani? Kumbuka huruhusiwi kutembea kwa zaidi ya mwendo wa umbali fulahi kwenye Sabato? Umewahi kufanya kazi yoyote siku ya Sabato? Kama jibu ni ndio, kwa nini?

Je, kutoa Fungu la Kumi (FlK) ni kati ya amri kumi za Mungu? Jibu ni hapana. Je, kwenye Agano jipya Wakristo wanafundishwa au kuhimizwa kutoa FlK? Jibu ni hapana.. Wengi tumefundishwa kuwa kutoa FlK ni AMRI na kutotoa ni hatia. Swali langu ni hili, nipe maandiko yanayoagiza hayo. Soma Biblia tafadhali, hata kama ni kusoma kitabu cha Malaki, kisome kitabu chote ukielewe. Soma Agano la Kale sehemu zinazozungumzia utoaji wa FlK.

"Mungu anasaidia wanaojisaidia" umewahi kusikia msemo huo? Wengi tumeusikia hivi: "Biblia inasema kuwa Mungu husaidia wanaojisaidia". Watu wengi, hata Wakristo pia, wanadhani kuwa msemo huu ni kweli na kwamba Biblia inasema hivyo. Hiyo ndio sababu ni muhimu kuisoma Biblia na kuielewa.

[color=indigo]“10 For whosoever shall keep the whole law, and yet offend in one point, he is guilty of all. 11 For he that said, Do not commit adultery, said also, Do not kill. Now if thou commit no adultery, yet if thou kill, thou art become a transgressor of the law.â€
User avatar
Berea
New member
 
Posts: 28
Joined: Tue Mar 22, 2005 2:06 pm

Postby Lydia » Wed May 17, 2006 9:53 am

kweli kuna maandiko nitatafuta muda lakini ningependa kusema hata Yesu mwenyewe alifundisha sana utoaji. angalia Luka 6:38 " wapeni watu vitu kipimo cha kujaa na kusindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Hii ina maana mlango wa kupokea ni kutoa sasa tukisema tumeokolewa kwa neema na kila kitu ni kwa neema basi tusifanye chochote inakuwa ni kinyume cha neno tunatakiwa kuwa watendaji pia na kuwa watendaji haina maana tunalipia wokovu hapana. Wagalatia 6:7 anasema "Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna. ili uvune ni lazima upande. Ili upate pesa lazima upande pesa. Hadithi ya Kornerio pia iko kwenye Agano jipya kwamba kwa sababu ya utoaji wake Mungu alipokea sala zake akamtuma malaika kumwambia kwamba sadaka zake zimefika mbinguni atume watu waende kwa Petro aje awabatize yeye na familia yake inamaana huyu alikuwa anatoa sadaka lakini alikuwa bado hajaokoka Mungu akaona sadaka peke yake hazitampeleka kwenye ufalme wa Mungu ila anahitaji wokovu
lakini kilichotangulia kwanza ilikuwa ni sadaka.

Agano Jipya halipingi Agano la kale, Yesu alisema sikuja kutangua torati bali kuitimiliza sasa hatuwezi kukataa yaliyopo kwenye Agano la kale. "Tunapookoka tunakuwa Uzao wa Ibrahimu na baraka hizo zinafuatana nasi haijalishi ziko kwenye Agano la kale au Agano Jipya.
Angalia Wagalatia 3:29,Wagalatia 3:13,14

Bado nasimama pale pale kutoa fungu la kumi ni agizo la Mungu (amri) na itolewe madhabahuni sio kupeleka kwa wajane hapo unakuwa hujafanya kitu kwa wajane peleka ya kwako ile fungu la kumi sio yako ni ya Mungu.
HALELUYA
User avatar
Lydia
Regular Member
 
Posts: 328
Joined: Fri Apr 29, 2005 7:11 am
Location: Mozambique

Postby Berea » Wed May 17, 2006 1:47 pm

Lydia wrote:Bado nasimama pale pale kutoa fungu la kumi ni agizo la Mungu (amri) na itolewe madhabahuni sio kupeleka kwa wajane hapo unakuwa hujafanya kitu kwa wajane peleka ya kwako ile fungu la kumi sio yako ni ya Mungu.


Dada Lydia, unachanganya mambo hapa. Mjadala hapa unahusu Fungu la Kumi na sio Kutoa (sadaka na kadhalika). Mkristo hana budi kutoa, ni agizo na ni himizo. Hata hivyo, huwezi ukatoa usichokuwa nacho. Hiyo ndio maana tunaambiwa kwenye Wakorintho wa Pili aya ya 9 msitari wa 7: "Every man according as he purposeth in his heart, [so let him give]; not grudgingly, or of necessity: for God loveth a cheerful giver." Toa unavyoweza. Toa vyote ulivyonavyo ukiongozwa kufanya hivyo na Roho wa Mungu. Kuna watu wengi kwenye historia ya Ukristo waliotoa vyote walivyokua navyo: kwa mfano mitume Stefano, Johana, na Paulo. John Huss na wengine walichomwa kwa moto wakiwa hai - the ultimate sacrifice.

Mimi binafsi nilikuwa mtoaji dhabiti wa FlK. Kaka yangu alipookoka alikuja kwangu baada ya miaka kadhaa na kutuomba tujadili swala hili la FlK. Kwangu mimi huo ulikuwa mzaha mkubwa. Hatukuwa na mjadala wowote. Kwetu sisi FlK ilikuwa ni amri kubwa na kutotoa ulikuwa kumwibia Mungu. Tulitoa 10% ya gross na sio net salary, yaani, mshahara kabla ya ushuru kutolewa. Nakumbuka wakati mmoja nilikuwa nalo fungu langu la kumi kwenye kituo cha basi. Mchungaji niliyemjua alitokea nikampa. Tukaenda pamoja kwenye kona na kuomba pamoja. Msamiati: Kutoa --> Giving, Sadaka (works - matendo); Fungu la Kumi --> Tithe (the law - sheria).

Dada Lydia, hebu nikuulize. Tuseme una fungu lako la kumi nyumbani. Huna hela yoyote isipokuwa hilo FlK. Jirani yako mgonjwa mahututi ukaijiwa usiku wa manane kusaidia na fedha ili apelekwe hospitali. Je, utaonyesha moyo wa upendo na kutoa hiyo fedha au utasema la hasha ... haiwezekani kamwe, FlK haliguswi.

Umesema unasimama pale pale kuhusu swala hili. Huo ni uamuzi wako na hiari yako. Nimeomba andiko au maandiko yanayo-support msimamo wako lakini hukutoa hata moja. Badala yake umesungumza tu kuhusu kutoa (kuna tofauti kubwa kati ya kutoa (giving) na FlK (thithing)). Biblia inasema imani bila matendo imekufa. Soma waraka wa Yakobo wa Pili... sisitiza kuanzia msitari wa kumi:

Ndugu zangu, mkiwa mnamwamini Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwabague watu kamwe. Tuseme mtu mmoja ambaye amevaa pete ya dhahabu na mavazi nadhifu anaingia katika mkutano wenu, na papo hapo akaingia mtu maskini aliyevaa mavazi machafu. Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: "Keti hapa mahali pazuri," na kumwambia yule maskini: "Wewe, simama huko," au "Keti hapa sakafuni miguuni pangu," je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya?

Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni! Mungu amechagua watu ambao ni maskini katika ulimwengu huu ili wapate kuwa matajiri katika imani na kupokea Utawala aliowaahidia wale wanaompenda. Lakini ninyi mnawadharau watu maskini! Je, matajiri si ndio wanaowakandamizeni na kuwapeleka mahakamani?

Je, si haohao wanaolitukana hilo jina lenu zuri mlilopewa? Kama mnaitimiza ile sheria ya Utawala kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu: "Mpende binadamu mwenzako kama unavyojipenda wewe mwenyewe", mtakuwa mnafanya vema kabisa.

Lakini mkiwabagua watu, basi, mwatenda dhambi, nayo Sheria inawahukumu ninyi kuwa mna hatia. Anayevunja amri mojawapo ya Sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja Sheria yote. Maana yuleyule aliyesema: "Usizini," alisema pia "Usiue". Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini lakini umeua, wewe umeivunja Sheria.

Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. Maana, Mungu hatakuwa na huruma atakapomhukumu mtu asiyekuwa na huruma. Lakini huruma hushinda hukumu. Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa? Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula. Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: "Nendeni salama mkaote moto na kushiba," bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?

Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa. Lakini mtu anaweza kusema: "Wewe unayo imani, mimi ninayo matendo!" Haya! Nionyeshe jinsi mtu anavyoweza kuwa na imani bila matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu. Je, wewe unaamini kwamba yuko Mungu mmoja? Sawa! Lakini hata pepo huamini hilo, na hutetemeka kwa hofu. Mpumbavu wee! Je, wataka kuonyeshwa kwamba imani bila matendo imekufa? Je, Abrahamu baba yetu alipataje kukubalika mbele yake Mungu? Kwa matendo yake, wakati alipomtoa mwanae Isaka sadaka juu ya madhabahu. Waona basi, kwamba imani yake iliandamana na matendo yake; imani yake ilikamilishwa kwa matendo yake.

Hivyo yakatimia yale Maandiko Matakatifu yasemayo: "Abrahamu alimwamini Mungu na kwa imani yake akakubaliwa kuwa mtu mwadilifu; na hivyo Abrahamu akaitwa rafiki wa Mungu." Mnaona basi, kwamba mtu hukubaliwa kuwa mwadilifu kwa matendo yake na si kwa imani peke yake. Ilikuwa vivyo hivyo kuhusu yule malaya Rahabu; yeye alikubaliwa kuwa mwadilifu kwa sababu aliwapokea wale wapelelezi na kuwasaidia waende zao kwa kupitia njia nyingine. Basi, kama vile mwili bila roho umekufa, vivyo hivyo imani bila matendo imekufa.


KIINGEREZA (New American Standard Bible)

My brethren, do not hold your faith in our glorious Lord Jesus Christ with {an attitude of} personal favoritism. For if a man comes into your assembly with a gold ring and dressed in fine clothes, and there also comes in a poor man in dirty clothes, and you pay special attention to the one who is wearing the fine clothes, and say, "You sit here in a good place," and you say to the poor man, "You stand over there, or sit down by my footstool," have you not made distinctions among yourselves, and become judges with evil motives?

Listen, my beloved brethren: did not God choose the poor of this world {to be} rich in faith and heirs of the kingdom which He promised to those who love Him? But you have dishonored the poor man. Is it not the rich who oppress you and personally drag you into court? Do they not blaspheme the fair name by which you have been called? If, however, you are fulfilling the royal law according to the Scripture, "YOU SHALL LOVE YOUR NEIGHBOR AS YOURSELF," you are doing well.

But if you show partiality, you are committing sin {and} are convicted by the law as transgressors. For whoever keeps the whole law and yet stumbles in one {point,} he has become guilty of all. For He who said, "DO NOT COMMIT ADULTERY," also said, "DO NOT COMMIT MURDER." Now if you do not commit adultery, but do commit murder, you have become a transgressor of the law.

So speak and so act as those who are to be judged by {the} law of liberty. For judgment {will be} merciless to one who has shown no mercy; mercy triumphs over judgment. What use is it, my brethren, if someone says he has faith but he has no works? Can that faith save him? If a brother or sister is without clothing and in need of daily food, and one of you says to them, "Go in peace, be warmed and be filled," and yet you do not give them what is necessary for {their} body, what use is that?
Even so faith, if it has no works, is dead, {being} by itself. But someone may {well} say, "You have faith and I have works; show me your faith without the works, and I will show you my faith by my works." You believe that God is one. You do well; the demons also believe, and shudder. But are you willing to recognize, you foolish fellow, that faith without works is useless? Was not Abraham our father justified by works when he offered up Isaac his son on the altar?

You see that faith was working with his works, and as a result of the works, faith was perfected; and the Scripture was fulfilled which says, "AND ABRAHAM BELIEVED GOD, AND IT WAS RECKONED TO HIM AS RIGHTEOUSNESS," and he was called the friend of God. You see that a man is justified by works and not by faith alone. In the same way, was not Rahab the harlot also justified by works when she received the messengers and sent them out by another way? For just as the body without {the} spirit is dead, so also faith without works is dead.


Asanteni na Mungu awabariki.
User avatar
Berea
New member
 
Posts: 28
Joined: Tue Mar 22, 2005 2:06 pm

Postby Lydia » Thu May 18, 2006 8:00 am

Kweli ndugu yangu Berea labda niseme mimi na wewe tumepata mafundisho tofauti kutoka kwa walimu tofauti. katika mafundisho mengi sana niliyopata kuhusu AMRI ya kutoa fungu la kumi moja wapo ni kutoka kwa mtumishi wa Mungu C. Mwakasege . Nimekopi kama ilivyo

TOFAUTI YA ZAKA NA DHABIHU

Kutokutoa zaka na dhabihu ni kumwibia Mungu. Mtu aliye mkristo asipotoa zaka na dhabihu anaitwa mwizi. Kuna wakristo ambao ni wezi lakini wao hawajui yakuwa ni wezi. Wamemwibia Mungu zaka na dhabihu. Mungu anasema hivi:

“Je! mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia ZAKA na DHABIHUâ€
HALELUYA
User avatar
Lydia
Regular Member
 
Posts: 328
Joined: Fri Apr 29, 2005 7:11 am
Location: Mozambique

Postby Berea » Thu May 18, 2006 8:32 am

Asante sana dada Lydia kwa hayo mafundisho. Nimeyasoma kwa ujumla. Mengi aliyoyaandika si mageni kwa sababu nimewahi kuyasoma kabla.

Nitayasoma tena mara ya pili kisha nikupe jibu langu. Ni vizuri kujadili mambo haya tunavyofanya ili kuyaelewa Maandiko ipasavyo.

Asante sana na Mungu akubariki.
User avatar
Berea
New member
 
Posts: 28
Joined: Tue Mar 22, 2005 2:06 pm

Next

Return to Maisha ya Kikristo

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 1 guest

cron