 |
amefufuka.com Come, let us reason together.
|
| View previous topic :: View next topic |
| Author |
Message |
Apostle of Jesus Member

Joined: 24 Sep 2007 Posts: 120 Location: Tanzania
|
Posted: Thu Oct 25, 2007 8:04 am Post subject: UHURU KATIKA KRISTO AU KUMUAIBISHA YESU? |
|
|
Dunia inabadilika lakini neno la Mungu lipo palepale! Mi Ningependa tujadili suala la mavazi ambalo wachungaji wanaogopa kulizungumzia kwa kuwaogopa watu.Manazi kama ilivyo kwa chakula ni hiari.Wapendwa tuwe wazi,Mungu ametuweka huru toka utumwa wa dhambi si vinginevyo!
sasa wapendwa tunaenda zaidi hata ya mataifa! inatisha!
Kumbu 22:5 inakataza kwa mwanamke kuvaa impasavyo mwanaume na kinyume chake.Lazima wapendwa tujue kuwa Mungu alitaka kuwe na utofauti kati ya mwanamke na mwanaume.Wengi wa wapendwa wanajitetea kuwa Mungu huangalia moyo! Si kweli,huangalia hata mwili(hekalu lake).Lazima ifike wakati tuachane na mambo ya ulimwengu huu.Kuokoka ni NJIA NYEMBAMBA,KUJIKANA MWENYEWE,KUJITWIKA MSALABA.....Kumbuka neno la Mungu linasema aupendaye ulimwengu hujifanya adui wa Mungu!
Sera ya dunia ya leo ni LOOK SEXY,FEEL SEXY,ACT SEXY.Kwa maana Nyingine Mwonekano wako,Fikra zako na matendo yako yawe ya ki-asherati au ki-zinzi.Mungu ametuitia utakatifu na sio uchafu.Hatupaswi kufuatisha tamaa za dunia hii.Utaniambia mwinjilisti unakosea.Mi navaa tu hakuna shida yoyote,hata hivyo sivai kumvuta mtu!
sawa lakini hebu tufuatane kujua tatizo la mavazi
Wakina dada na akina mama:
Kabla sijazungumzia chochote lazima tujue kuwa ukiwa utupu ni rahisi kwa mtu kutoendelea kukuangalia (aliyeokoka).Ni tabia ya mwili wa mwanaume kutamani kuona zaidi pale anapoona kasehemu kadogo tu ka sehemu fulani za mwanamke.Sehemu hizo ni kama matiti,mapaja,kitovu,kiuno,mgongo..n.k. Shetani kwa kulijua hilo,na kwa kukutumia ma-ajenti wake katika viwanda vya nguo amewateka akina dada wengi,asilimia kubwa wakiwa wapendwa!Hebu tuwe wazi wapendwa,kama gauni ni nguo ya kike na hakuna ubishi juu ya hilo,ni vipi suruali iwe ni nguo ya kike na kiume? Ukitazama kwa makini Kumb 22:5 utaona kuwa Mungu hataki kuwe na vazi ambalo ni la jinsia mbili.asili ya mavazi ya aina hii ni utamaduni wa hiphop ambao si wa kikristo na haukubaliki na wakristo(nikisema wakristo namaanisha walio wa kristo-yaani waliookoka)!Pia unatokana na Feminism movements(sijui kiswahili chake)ambao wanadai kuwa sawa na wanaume(sawa nalusifa alivyotaka kuwa sawa na Mungu)Hivyo si sawa kwa mlokole kuvaa suruali,ni vazi la kiume.Halafu vimini ndugu zangu,ni aibu.Hebu fikiri hili:Yesu alisema mtu akimtamani mwanamke amezini naye moyoni.Sasa fikiri kwa kuvaa kimini watu wangapi wamezini nawe mioyoni mwao? Je unafikiri uta kwenda Mbinguni kwa kuwakwaza hao waliozini nawe mioyoni mwao? Kwa hiyo mpaka hapa suruali,vimini,vitopu si sawa kwa mkristo.Halafu kuna mavazi ambayo yamepata umaarufu hivi karibuni.Unakuta mtu amevaa gauni reeefu mpaka miguuni.Halafu limechanwa mpaka juu ya magoti(mpasuo),kisha limebana hipsi na makalio na sehemu nyingine zipo loose.Tena sehemu ya matiti imeachwa wazi kidogo kama robo hivi.Kwenye mabega imechanwa au ina matundu na mgongo uko wazi.Hiv wapendwa hatujiulizi?Mpasuo maana yake nini?Kw nini uichane nguo yako?Ili uonyeshe nini?Tuacheni kumwaibisha kristo.
Na mwisho utakuta nguo ndefu lakini inaonyesha ndani(pamba nyepesi).Hili ni critical! kwa mkristo halikubaliki!
Halafu naomba niulize,wakina dada,Mungu alipoumba alisema yote ni mema,sasa hivi vitendo vya kujibadilisha sura nywele....ni kwa sababu African are never beautiful?
Wanaume na akina kaka:
Mstari huohuo unaelezea akina kaka kutovaa yawapasyo wanawake.Ajabu na kweli ni kuwa unaweza kusalimia jamani akina dada habari zenu,mmoja wao akanuna.Baadaye utakuja tambua kuna mwanamume kati yao!Hivi kitendo cha wanaume kusuka ni cha ki-Mungu?
Hapana! Hata biblia imeandika wanawake ndio hujipamba kwa kusuka,sasa vipi mwanume ndio asuke.Na wengine ni wapendwa kabisa.Hebu tuache kuchezea wokovu wa thamani kiasi hiki.Heleni masikioni,bangili mikononi,cheni shingoni na mabo yote ya kike tuwaachie wanawake.Tujue kuwa utamaduni wa hiphop haukutoka kwa Mungu wetu hivyo tuachane na namna ya dunia hii tumwelekee Mungu.
Mungu ametuweka tuwe taa ya ulimwengu na chumvi ya ulimwengu.Hivi leo si ajabu kuona mpendwa akiwa nahali mbaya ya kimavazi zaidi ya asiyeokoka! sasa hiyo chumvi iko wapi? Unaweza kukutana na akina kaka ukafikiri ni wahuni fulani kumbe eti ni walokole,he tunaenda wapi?
Hivi yesu aliposema atatuweka huru alimaanisha uhuru wa kufanya kia tutakalo? Je yesu alikuja kutengua sheria ili tuwe huru? Sivyo hata kidogo,Yesu alitupa ushindi juu ya dhambi,ili tuifanye sheria kwa furah,maana si sheria tena bali ni namna yetu ya maisha.Kuishi sawa na neno ndio ushindi aliotupatia Yesu.Ukiona watu wanakuona sawa na mataifa jiangalie kama upo bado katika msingi wa kristo
Mwisho nawaasa wakristo,ANGALIA ASILI YA KILA JAMBO KABLA YA KUJIINGIZA MAANA MUNGU HATAJENGA JUU YA MSINGI WA SHETANI
Mbarikiwe, Mwinjilisti Stephen MD _________________ For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men, Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly |
|
| Back to top |
|
 |
chibe New member
Joined: 19 Oct 2007 Posts: 4 Location: Arusha-Tanzania
|
Posted: Fri Nov 09, 2007 10:04 am Post subject: Re: UHURU KATIKA KRISTO AU KUMUAIBISHA YESU? |
|
|
Ulichoongea mwinjilisti ni cha kweli kabisa na wadada wanasema eti wanaume sisi ndo wenyeshida,mbona wazungu wanavaa nguo fupi na bado kwao haina shida?nani kawadanganya kwamba kwaao hainashida,ina shiada vilevile na tena wao ndo wanajua namna ya kuwateka wanaume.
Na nikwambie mwanamke yeyote anayevaa nguo fupi ukimuuliza kwa taratibu atakwambia siri iliyopo,ni kuwafanya wanaume wasihangaike kujua yeye yukoje kwa ndani.tena wanasema wateja wao wakija wanakuwa hawana shida ya kuanza kuchunguza ni yupi wa kuchukua.
Lakini ndugu hao ni watu ambao hawajaokoka na wameamua kwa hiyari yao kufanya hiyo biashara,wewe umeokoka dada kwa nini ujiingize kwenye biashara isiyo yako.
Nawaomba tuuhemu wokovu tuliopewa na Bwana Yesu.
Mbarikiwe
Chibe, _________________ Stanley George Ala Chibelenje
Istitute Of Acountancy Arusha
P.O.Box 2798
Phone +255 27 2506605
Mob:+255 713 727056
E-mail schibelenje@iaa.ac.tz
Website:www.iaa.ac.tz |
|
| Back to top |
|
 |
Apostle of Jesus Member

Joined: 24 Sep 2007 Posts: 120 Location: Tanzania
|
Posted: Sun Nov 18, 2007 8:49 am Post subject: Kwa utkufu waYesu tu! |
|
|
Nilikuta watoto wa kama form one hivi wako wanaangalia web moja ya wanamitindo:Huku wakiwasifu wamependeza sana.Hii ilinishtua kwa sababu wale watu ktk hiyo website walikuwa wamevaa vinguo vya ajabu mno! Nilichojifunza:Hizi nguo asili yake si Mungu.Hebu naomba nifahamu;kama tukisema zimetoka kwa Mungu Kumb 22:5 Ni ya nini? watoto wa Mungu wengi wanalia"Ni kipindi cha neema!"Lkini Yesu Mtoa neema hakusema popote kuwa ameiondoa hiyo sheria!
Kwa kila neno au tendo (pamoja na mavazi) tufanye kwa utukufu wa jina la Yesu!
Mbarikiwe
Mwinjilisti Stephen
Dar es salaam
Tanzania _________________ For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men, Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly |
|
| Back to top |
|
 |
sinmm Site Admin

Joined: 16 Aug 2004 Posts: 432 Location: Scandinavia
|
Posted: Tue Nov 20, 2007 1:56 pm Post subject: |
|
|
Mwinjilisti Stephen, unayosema ni ya kweli na ukienda ulaya au marekani utajikwaa. Utawaona wavulana 'waliookoka' wamesuka nywele na wengine wametoboa masikio. Wakati wa joto (summer) watu wanavaa mavazi ya kushangaza, hata kanisani.
Si adimu kuwaona wanaume wamevaa kaputula na T-Shirt wakienda kanisani wakati wa summer. Ni vigumu mno kupata wasichana/wanawake wasiovaa suruali, hata wake wa wachungaji. Mada hii tumeizungumzia sana hapa zamani; hasa wanawake kuvaa suruali. Kuna nchi fulani utapata ni kawaida wanaume kuvaa sketi (au nguo zinazofanana na sketi); kwa mfano Scotland, Malaysia, nk. |
|
| Back to top |
|
 |
Apostle of Jesus Member

Joined: 24 Sep 2007 Posts: 120 Location: Tanzania
|
Posted: Fri Nov 23, 2007 8:49 am Post subject: UHURU WA YESUUUU! NI WA KWELIIIIIIII! |
|
|
Lakini KAKA sinmm hilo halihalalishi kuvunja sheria ya Bwana.Kumbuka Mungu aliangamiza dunia na kuacha familia ya nuhu pekee.Watu wengi kufanya jambo fulani haimbadilishi Mungu wala sheria yake! Ni chaguolAKO WEWE mkristo kumtii Mungu au kufuata wanadamu.Kwa Mungu hakuna wengi wape.Pia kuhusu wanaume kuvaa sketi,Mungu hakuwa specific ktk mavazi.Alituacha tuchague wenyewe.Lakini neno linasemaje? MWANMKE ASIVAE YANAMPASA MWANAMUME NA MWANAMUME VILEVILE YASIYOMPASA! Kama wanaume wakivaa sketi na wanawake suruali NO PROBLEM! lakini haiwezekani kuvaa vazi ambalo ni universal.Kwa Mungu halipo.Mpo hapo wapendwa!
Mbarikiwe
-----Unampenda Yesu? Mtumikie!-------- _________________ For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men, Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly
Last edited by Apostle of Jesus on Wed Dec 05, 2007 1:51 pm; edited 1 time in total |
|
| Back to top |
|
 |
sinmm Site Admin

Joined: 16 Aug 2004 Posts: 432 Location: Scandinavia
|
Posted: Fri Nov 23, 2007 1:56 pm Post subject: |
|
|
Bwana asifiwe!
Asante sana Stephen kwa mawazo yako. Kwanza, sahihisho; sinmm si mwanamke ni mwanamme.
Kweli, Mungu habadiliki. Yeye ni Yule Yule, jana, leo na milele. Kuhusu mavazi, umesema, " MWANMKE ASIVAE YANAMPASA MWANAMUME NA MWANAMUME VILEVILE YASIYOMPASA! Kama wanaume wakivaa sketi na wanawake suruali NO PROBLEM! lakini haiwezekani kuvaa vazi ambalo ni universal". Hapo kuna tatizo, hasa tukizingatia uvaaji wa suruali.
OK. Kwanza: tuseme dada MvaaSuruali amehama kutoka kwao na kutulia kwenye bara au nchi isiyoruhusu kinadada kuvaa suruali (dunia leo ni global village). Je, aendelee kuvaa suruali au abadili mtido na kuvaa sketi tu sasa?
Pili, uvaaji wa suruali ulianza lini na wapi? Inakubalika, na ukweli wa mambo, hasa kwetu sisi waafrika, kuwa mavazi ya kisasa (suruali, kaputula, sketi, n.k.) yalitufikia katika miaka ya juzi tu. Wakoloni walipowasili, babu na bibi zetu walijisitiri kwa kutumia ngozi za wanyama kama ng'ombe na mbuzi, migomba ya ndizi au makuti ya mnazi. Wengi, narudia ... wengi walikwenda uchi na hawakuona haya. Hata sasa, kuna makabila mengi tu duniani wanaokwenda uchi.
Tatu, tukishathibitisha ni lini na wapi uvaaji wa suruali ulianza, itakuwa vizuri kujua ni nani aliyetoa uamuzi wa wanawake au wanaume kuvaa suruali.
Inawezekana Kumbukumbu 22:5 ilipoandikwa watu wakati huo walivaa mavazi tofauti kabisa na tunayovaa sasa. Kwenye picha na filamu inayochora maisha yalivyokuwa wakati huo, tunaona wanawake wamevaa marinda ilhali wanaume wamevaa kanzu ndefu.
Kwenye maduka ya nguo za kinamama utaona kuwa kuna sehemu za suruali, sketi, marinda, na kadhalika. Mwanamme akinunua suruali kwenye sehemu hii na kuivaa haitamtosha vizuri kwa sababu mwili wa mwanamke ni tofauti sana na mwili wa mwanamme.
Haya ni mawazo yangu mimi. Sijui wengine wanasemaje. |
|
| Back to top |
|
 |
Binti Sayuni New member
Joined: 20 Dec 2007 Posts: 14 Location: DAR ES SALAAM
|
Posted: Thu Mar 27, 2008 2:56 pm Post subject: |
|
|
yaani jamani mie haya mpaka sasa huwa yananischanganya, kwani watu hata watumishi wa Mungu wamekalia kimya mambo haya, wengi wao hawakemei, jamani hivi tunaenda wapiiii? _________________ The Lord is my Light and my salvation; whom then shall I fear |
|
| Back to top |
|
 |
Apostle of Jesus Member

Joined: 24 Sep 2007 Posts: 120 Location: Tanzania
|
Posted: Fri Apr 04, 2008 9:53 am Post subject: |
|
|
| Binti Sayuni wrote: | | yaani jamani mie haya mpaka sasa huwa yananischanganya, kwani watu hata watumishi wa Mungu wamekalia kimya mambo haya, wengi wao hawakemei, jamani hivi tunaenda wapiiii? |
2Wakorintho 1:2-4,12- [soma sura yote]
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu;kwa kuwa naliwaposea mume mmoja,ili nimletee Kristo bikra safi. Lakini nachelea kama yule nyoka alivyodanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikra zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye akiihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri au mkipokea roho nyingine msiyoipokea......Lakini mimi nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi;ili kwamba katika neno hilo waonekane kama sisi.maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu. Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
Dada upo hapo! Watumishi wa Yesu yupi? Mtu atavaa hivi ukimweleza ukweli atasema mbona mtumishi fulani...!!
Jamani Kuna Yesu mwingine na wapo wengi tu! Yesu wa Biblia hasemi tuvae mavazi ili kufanana na watu wa mataifa. Si haki kusema Yesu nakaubalina na visuruali vya Jeans ambavyo dada zetu wanavaa
Ni watumishi wa shetani waliojigeuza wa Mungu ndio watasapoti vitu hivyo kwa kisingizio cha neema. Nilipata bahati ya kupita Jengo moja la nguo. Nikakuta modeli mbalimbali zikionesha namna nguo husika ilivyokusudiwa kuonekana kama mhusika atavaa. Ilinitisha kuona modeli ya suruali ikiwa na sanamu liloivaa likiwa linatingisha makalio!! Hilondilo kusudi languo hizo. Kuonesha maumbile ambayo Mungu alikusudia ayaone mume wako tu. Mwili wako ni zawadi kwa mumeo na si kila mtu. Naamini watumishi wa shetani ni wengi kuliko wa Mungu ktk siku za leo
Kwa taarifa yenu, makampuni kadhaa ya nguo niliyotafiti yanamilikiwa na waabudu mashetani, na wanamuziki wanaoongoza kwa kumchukia Yesu! Unatarajia nini toka kwao?? Ushauri wangu:Tafuta ngu ya KIKRISTO dukani, ukikosa KASHONE kwa Mafundi cherehani!!
Hivyo natarajia kama wewe ni mtoto wa Yesu, nikikuuliza mbona unafanya hivi? Natarajia uniambie: Mbona Yesu alifany? Na si mtu mwingine
Mbarikiwe na Yesu
Mwinjilisti Stephen _________________ For the grace of God that bringeth salvation hath appeared to all men, Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly |
|
| Back to top |
|
 |
Binti Sayuni New member
Joined: 20 Dec 2007 Posts: 14 Location: DAR ES SALAAM
|
Posted: Wed Apr 09, 2008 8:44 am Post subject: |
|
|
Mwinjilisti Stephen nashukuru sana kwa ufafanuzi wako, tena nimelewa sana na ubarikiwe. Watu wengi haswa waamuni wanaangamia kwa kukosa maarifa, wengi wao hata kusoma biblia hawasomi, wamebanwa na mambo ya kidunia. naamini kuwa ule mwisho umekaribia :roll: _________________ The Lord is my Light and my salvation; whom then shall I fear |
|
| Back to top |
|
 |
|
|
You cannot post new topics in this forum You cannot reply to topics in this forum You cannot edit your posts in this forum You cannot delete your posts in this forum You cannot vote in polls in this forum
|
Powered by phpBB © 2001, 2005 phpBB Group
|